Posts
Showing posts from April 4, 2017
EWURA yatangaza bei mpya za mafuta
- Get link
- X
- Other Apps
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia kesho, huku mafuta ya petroli yakionekana kushuka. Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa zimebadilika ikilinganishwa na beo za Machi Mosi mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita sawa na asilimia 0.29. Aidha Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21. "Hii shilingi tatu inaweza kuonekana ni ndogo lakini ina impact () kubwa sana kwa jamii, kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la d...
TRA yakusanya kodi jumla kuu soma hapa ..TATA BLOG nimekufikishia
- Get link
- X
- Other Apps
Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya kodi ya jumla ya Sh. Trilioni 10.87 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2016/17 ambapo makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa makusanyo ya asilimia 9.99 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi, Richard Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inawashukuru walipakodi wote ambao wameitikia wito. “TRA inatoa wito kwa kila mlipakodi kuwajibika kulipa kwa wakati pamoja na kufichua wale wasiotimiza wao kikamilifu,”amesema Kayombo. Aidha, pamoja na mafanikio hayo kwa kipindi cha miezi tisa Mamlaka hiyo itaelekeza juhudi zake katika kukusanya kodi mbali mbali ili kuhakikisha lengo la mwaka la kukusanya Trilioni 15.1 linafikiwa. Hata hivyo, amesema kuwa TRA inazidi kusisitiza matumizi mashine za EFD pamoja na zoezi la uhakiki wa TIN katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani linaendelea hivyo wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanatumia m...
Kauli ya ACT Wazalendo kuhusu Rais Magufuli kumteua Mwanachama wao , Prof. Kitila Mkumbo Kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji
- Get link
- X
- Other Apps
Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu. Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu. ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na ...
Polisi yaua majambazi
- Get link
- X
- Other Apps
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia. Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi. “Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “ “Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga. Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha ...