Posts

Showing posts from May 16, 2017

Mwanafunzi akishitaki chuo kikuu cha UDSM

Image
Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Alphonce Lusako, amewasilisha maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, aruhusiwe kukishtaki chuo hicho kwa kumkatisha masomo. Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya sheria alifukuzwa baada ya kufutiwa usajili Januari 26, pamoja na mambo mengine akidaiwa kusajiliwa kwa makosa kwasababu aliwahi kufukuzwa chuoni hapo. Lusako anayewakilishwa na Wakili Jebra Kambole anaiomba Mahakama impe kibali cha kuishtaki UDSM na itoe amri ya kuzuia uamuzi wa kumfutia usajili. Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Mei 23 na Jaji Pellagia Khaday. Lusako alijiunga na UDSM kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akiwa amedahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu. Hii ni mara ya pili kwa Lusako kufukuzwa chuoni hapo, mara ya kwanza ni Desemba 13, 2011, pamoja na wenzake kadhaa, akiwa mwaka wa tatu walifukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu nchini wakidaiwa kuratibu mgomo wa wanafunzi UDSM. Hata hivyo, anadaiwa alikuwa akip...