Mwenge wa uhuru umewasili jijini mbeya na utakimbizwa kwenye wilaya 7
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Amos Makalla ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Songwe mapema jana,jijini humo huku vifijo na nderemo za kuwasili mwenge huo vikiwa vimeshamiri,Hafla ya kuupokea Mwenge huo imefanyika Wilayani Chunya April 16,2017.Mwenge huo ukiwa mkoani Mbeya utakimbizwa katika halmashauri saba,ambapo utafanya kazi ya kukagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiupokea Mwenge wa Uhuru wilayani Chunya mkoani Mbeya sambamba na kula kiapo cha kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri zote za mkoa wa Mbeya. Baadhi ya makamanda wa jeshi la Polisi ambao pia ni miongoni Mwa wakimbiza mwenge wa Uhuru uliowasali hapo mkoani Mbeya Baadhi ya wanachama na Wafuasi wa Chama cha Mapindizi (CCM) sambamba na viongozi wa chama wakisherehekea mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru ulio wasili jana April 16,2017 mkoani Mbeya na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa Mbeya...