Posts

Showing posts from April 20, 2017

NIRAHISI SASA KUIPATA SIMU ILIYO IBIWA AU KUPOTEA

Image
Leo nakusogezea hii Kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia sasa tunaweza kusema , Wezi Wa simu watapungua na wengiwao watakamatwa Kama ulishawahi kuibiwa simu au umepoteza simu hii inaweza kukusaidia sasa kuipata simu yako au kuizuia isifanye   chochote huko ilipo ama kufuta kabisa data zote zilizopo huko ilipo ilikukufanya wewe uwe salama kabisa . Kama unahitaji huduma hizi   hakikisha unakumbukumbu  sahihi ya email yako na password yako ambayo umeitumia kufungulia google account , ili kufanikisha zoezi zima   . unatatizo tupigie kwa namba 0655801621 kwa maelezo zaidi na huduma pia

Ada kulipwa kwa kutumia mbuzi na kondoo huko nchini.....

Image
Wazazi nchini Zimbabwe ambao hawawezi kugharimia karo ya shule wanaweza kupeleka mifugo wao kama mbuzi na kondoo kama malipo, waziri mmoja amesema. Waziri wa elimu nchini Lazarus Dokora aliiambia gazeti la Sunday Mail kuwa itabidi shule zilegeze masharti yao ya kudai karo ya shule kutoka kwa wazazi, na pia kando na mifugo wanaweza kubali kupewa huduma na ujuzi kama malipo. "Ikiwa kuna mwashi au mjenzi katika jamii, yeye yuapaswa kupewa ile nafasi ya kufanya kazi kama njia ya kulipa karo," gazeti lilimnukuu. Kuna shule ambazo tayari zinakubali mifugo kama malipo, Sunday Mail linasema. Hata hivyo afisa katika wizara hiyo alifafanua kwamba wazazi ambao wanaweza kulipia watoto wao karo kwa mifugo ni wale wa mashambani, lakini wazazi walioko mijini wanaweza kulipa kutumia njia nyingine kama vile kuifanyia shule kazi fulani. Tangazo hilo lilitolewa baada ya Zimbabwe wiki jana kupendekeza watu waruhusiwe kutumia mifugo yao kama mbuzi, ng'ombe na kondoo kama rehani wanapoch...

Matumizi madogo ya pesa hufanikisha mambo makubwa ,jifunze hapa

Image
Katika maisha ya kawaida ya Watanzania tulio wengi, kwa namna moja ama nyingine umewahi kusikia au wewe binafsi kulalama kuwa pesa yako haikai au haiendi kama unavyotegemea. Hiki ni kilio cha kawaida ambacho hakitokani na kutapanya fedha bali kutojua mbinu sahihi ya kawaida tu ya kuzitumia vyema pesa ‘kidogo’ kupata matokeo makubwa. Moja kati ya tabia ya fedha hasa hizi tunazopata watu wa kima cha chini ni kwamba huwa ni kama zinayaita matatizo au matumizi, pindi tunapokuwa nazo. Yaani mambo yanaweza kwenda tofauti na ulivyokuwa umepanga, matumizi yanaongezeka kidogo-kidogo ila unashtuka umebaki na kisalio ‘kiduchu’ au hata umefilisika kabisa. Ndio hapo kilio cha ‘mishahara haikutani’ kinazidi. Leo tutakupa mbinu ya namna ya kubadili kidogo mtindo wako wa maisha bila kujibana bali kubana mianya ya kutumia fedha zako bila kufuata mipango uliyojiwekea. Epuka vishawishi vya ATM, Simu Pesa : Jitahidi mara kadhaa kukwepa kutembea na ATM au kuweka ...

Waalimu wa kiswahili Tanzania kupata ajira rwanda

Image
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba. Pamoja na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi na teknolojia. Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo