Posts

Showing posts from May 18, 2017

RAIS ZUMA ATAKA ZIWA VICTORIA LIBADILISHWE JINA

Image
.  Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo. Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo. Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria. Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema  Ziwa hilo kuendelea kuitwa  Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao. “Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango  dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma