Wakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wakipatikana juzi usiku, suala la wawakilishi wa upinzani limetawaliwa na hali ya kutoeleweka, huku ikibainika rasmi kuwepo kwa CUF “A” na CUF “B”. Kikao cha juzi kilichotawaliwa na mjadala wa kikanuni kuhusu wawakilishi wa Chadema na CUF, kiliweka rekodi ya kuchukua muda mrefu baada ya kumalizika saa 7:00 usiku kikikipiku kikao kilichojadili sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow. Bunge lilichagua wanachama sita wa CCM kuingia Bunge la Afrika Mashariki, pamoja na mmoja kutoka CUF, ambaye amezua mjadala baada ya jina lake kukubaliwa na msimamizi wa uchaguzi licha ya kusainiwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho badala ya katibu mkuu ambaye aliwasilisha jina jingine. Waliopitishwa ni Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe na Alhaj Adam Kimbisa kutoka CCM, wakati Habib Mnyaa, aliyeku...