ACT WAZALENDO NA VYETI FEKI
CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeitaka Serikali kufanya uhakiki wa vyeti kwa viongozi wote wa siasa na isipofanya hivyo kitafikisha suala hilo mahakamani. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema endapo Serikali haitawahakiki viongozi hao na mamlaka zinazohusika kutowachukulia hatua kwa kughushi vyeti, kitafungua mashtaka mahakamani. “Malalamiko ya wananchi kuwa kuna viongozi wamatumia vyeti feki na wengine wakituhumiwa kuwa na shahada batili ni ya muda mrefu. “Ikumbukwe kiongozi ni kama dereva kwa hiyo kuwaacha kwa kisingizio cha kujua kusoma na kuandika ni sawa na kuwa na dereva ‘kihiyo’ anayeendesha gari lililo na abiria waelewa,” alisema Shaibu. Alisema kitendo cha kutowahakiki viongozi hao kinapotosha mantiki nzima ya mchakato wa uhakiki na kuweka upendeleo wa dhahiri baina ya watumishi wa umma. “Msingi wa mchakato huu ni kuhakikisha t...