Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika mikoa yote 31 Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi jana katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku 195. Katika sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar. Kiongozi huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi). Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU' Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali hiyo Dkt. A...