Posts

Showing posts from April 14, 2017

Mwimbaji wa nyimbo za injili ahukumiwa ,kosa lake fahamu hapa

Image
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya milioni moja , Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.   Mwasote, ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa injili.   Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.   Awali, Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Injili.   Hakimu Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili apangiwe shughuli ya kufanya

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

METHALI MIA SITA NA KUMI ZA KISWAHILI (610) METHALI MIA SITA NA KUMI (610) 1. Aanguaye huanguliwa. 2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu. 3. Abebwaye hujikaza. 4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti. 5. Adui aangukapo, mnyanyue. 6. Adui mpende. 7. Adui wa mtu ni mtu. 8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna. 9. Ahadi ni deni. 10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 11. Akiba haiozi. 12. Akili ni mali. 13. Akili ni nywele kila mtu ana zake. 14. Akili nyingi huondowa maarifa. 15. Akutukanae hakuchagulii tusi. 16. Akipenda chongo huita kengeza. 17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki. 18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema. 19. Akupaye kisogo si mwenzio. 20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda. 21. Alisifuye jua, limeuangaza. 22. Aliye juu msubiri chini. 23. Aliye kando, haangukiwi na mti. 24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi. 25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua. 26. Akufukuzae hakwambii toka. 27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa. 28. A...