Marekani haitaivumilia tena Korea Kaskazini
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema kipindi cha taifa hilo kuwa na subira na Korea Kaskazini kimepita. Bw Pence alisema hayo alipozuru eneo ambalo haliruhusiwi kuwa na wanajeshi katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini. Ziara yake imetokea kipindi ambacho hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika rasi ya Korea, huku Marekani na Korea Kaskazini zikijibizana vikali. Bw Pence aliwasili mjini Seoul Jumapili saa chache baada ya Korea Kaskazini kutekeleza jaribio la kurusha kombora, ambalo halikufanikiwa. Jumatatu, Marekani na Korea Kusini zilianzisha mazoezi ya pamoja ya majeshi yake ya wanahewa, kuhakikisha kwamba wanajeshi wake wako tayari kwa tishio lolote kutoka kwa Korea Kaskazini, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kusini. Bw Pence, ambaye babake alipigana katika Vita vya Korea, alikuwa akihutubu katika kijiji cha Panmunjom siku ya Jumatatu. Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini Korea Kaskazini yaonywa na Marekani Nani alimrukia Kim Jong-un? Ni katika k...