Waziri mwakyembe apiga marufuku kusomwa kwa magazeti katika redio na televisheni
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza. Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia. Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC