Posts
Showing posts from April 6, 2017
Wema amfungukia hamo....zaidi soma katika blog
- Get link
- X
- Other Apps
Malkia Wema Sepetu amemjibu rapper Harmorapa juu ya ujumbe wake aliouandika wiki iliyopita kwenye mtandao wa Instagram kuwa akifanikiwa kumpata mrembo huyo atatangaza ndoa na kumtimizia kila anachokihitaji. Wema ameibuka na kuamua kumjibu msanii huyo na kumwambia kwa anamuheshimu sana na kama inawezekana atafute mtu ambaye anaendana nae. Kupitia ukurasa wake wa instagram,Wema ameonekana kukasirishwa na ujumbe huo na kuamua kumuandikia barua yene ujumbe mzito chipukizi huyo anayekuja kwa kasi. Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima y...
Upinzani kenya waruhusiwa kujihesabia kura ...zaidi soma kwenye tata blog
- Get link
- X
- Other Apps
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imekubali hitaji la vyama vya kisiasa kujihesabia kura katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika Agosti 8, mwaka huu. Hata hivyo, licha ya ruhusa hiyo tume hiyo imesema kuwa ni yenyewe pekee yenye ruhusa na mamlaka ya kutangaza matokeo ya mwisho. Awali Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa NASA, utaratibu kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo. Viongozi wa upinzani wanasema kuwa uwepo wa kituo hicho utasaidia kuzuia udanganyifu katika uchaguzi huo. Rais Uhuru Kenyatta anawania muhula wa pili wa uongozi wake na anatarajia kuukabili muungano wa vyama vikuu vya upinzani. Uamuzi wa tume ya uchaguzi Kenya umekuwa tofauti na ilivyokuwa Tanzania ambapo Muungano wa Vyama vya Upinzani ‘UKAWA’ ulibuni kituo chake cha kuhesabia kura lakini hakikuruhusiwa kufanya kazi yake hadi mwisho huku baadhi ya wahusika wakitiwa nguvuni ...
Aliye muweka mpenzi wake kwenye jaba la maji sasa mikononi mwa..,zaidi soma hapa
- Get link
- X
- Other Apps
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba. Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka. Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema; “Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia wata...
Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania akutana na balozi wa israel hapa nchini leo jijini dar es salaam
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan baada ya kutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017 PICHA NA IKULU
Spika wa bunge aagiza halima mdee akamatwe ,mbowe nae afike kamati ya maadili
- Get link
- X
- Other Apps
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo wa EALA. Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo na anatakiwa kufika leo.
Roma mkatoliki akamatwa
- Get link
- X
- Other Apps
Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana. Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio. Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records. "Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa
MBUNGE WA MTAMA NAPE NAUYE KUUANIKA UKWELI JUMAMOSI HII
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa Jumamosi April 8, 2017 atakuwa jimboni kwake ambapo atazungumza na wapiga kura wake kuwaeleza ukweli wa mambo yaote yaliyotokea. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nape Nnauye amendika kuwa, “ Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki . Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE . Ni Jmosi hii tar 8/4/17.” Nape aliondolewa kwenye nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Nape aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais alitengua uteuzi wake na kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape. Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia ha...
HAPPY BIRTHDAY KWAKO
- Get link
- X
- Other Apps
Nijambo njema kuongeza namba ya miaka ulioishi duniani sio wote walioweza kutimiza umri AMBAO Leo ukonao ni rehema ya MWENYE ENZI MUNGU kukufikisha Siku ya Leo wewe nimtu wapekee sana katika hii dunia ndio maana hata alama za viganja vya mikono yako havifanani na mwingine Zaidi nikutakie mafanikio katika kazi yako ya uandishi Wa VITABU MBALIMBALI nya mashairi ya kiswahili na mwaka huu ukawe mwaka Wa viwango vipya katika kila jambo ulifanyalo kiroho,kimwili,na kiakili