Posts

Showing posts from April 25, 2017

Maandalizi ya Sherehe za muungano yafikia kilele

Image
April 26/04/19964 Zanzibar na Tanganyika ziliungana kupitia kupitia wasisi wake Julius kambarage nyerere na rais  Wa Zanzibar ,katika kuadhimisha sherehe hizo taasisi mbalimbali zimeandaa matembezi ya amani  kama moja ya kukumbuka waasisi wetu Mhadhiri Wa chuo kikuu Ajuco songea akihamasisha wanafunzi na wanajumuiya wengine amesema " Watu wote mnakaribishwa kushiriki mazoezi ya matembezi katika kuazimisha siku kuu ya muungano hapo kesho. Matembezi yataanzia chuoni Ajuco na kuishia mletele (Namtumbo road) na kurudi hadi chuoni kuanzia saa kumi na mbili na nusu. Mahali kukutana ni chuoni Ajuco, kila mmoja wetu anakaribishwa kushiriki matembezi hayo katika kuimarisha afya zetu. Hii si ya kukosa na ni zaidi ya kupanda mlima matogoro. " Aliyasema hayo kupitia kundi la  AJUCO COMMUNITY  mapema hii Leo.

WAZIRI MSTAAFU NAPE NAUYE AMEYAANDIKA HAYA

Image
Usiku wa kuamkia Leo  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM. “Watu wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE. “Bahati niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema, mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi”  Ameandika  Nape