HISTORIA FUPI IKIMUHUSISHA MAREHEMU CHANDE KIONGOZI WAO
Mtego wa Freemasons ulikua hivi Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’. Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki. Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo. Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania. Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili mi...