Posts

Showing posts from May 2, 2017

Marekani waanza upya kuichokonoa korea

Image
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea. Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini. Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini. Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang. Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera. Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi

Mbunge wa kawe Halima mdee asimamishwa rasmi kutohudhuria vikao ...zaidi soma hapa

Image
Mbunge wa jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee amepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vya bajeti katika bunge linaloendele hivi sasa Dodoma kufuatia Mbunge huyo kubainika kuwa alitukana bungeni, lakini Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani amesamehewa.  Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Mhe. Freeman Mbowe kwa kudharau mamlaka ya spika na kumsamehe kosa lake hilo kwa kile lichosema kuwa lilikuwa ni kosa la kwanza kwa kiongozi huyo kufanya.  Akisoma uamuzi huo, mjumbe wa kamati, Almasi Maige amesema Bunge lijadili na kutoa uamuzi kwa kiongozi huyo kusamehewa kwa sababu ni kosa la kwanza na aliitikia wito bila usumbufu na aliomba radhi, hivyo bunge limeazimia kumsamehe.  Mambo yamekuwa magumu kwa kwa upande wa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ambapo bunge limeazimia mbunge huyo kutohudhuria vikao vya bunge la bajeti vyote vinavoendelea sasa kwa kosa lake la kumtukana Spika na Mbunge akiwa bungeni.  Halima...