BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YAPANGA KUTANGAZA VIGEZO VIPYA VYA WANUFAIKA MWAKA 2017/2018

B odi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ( HESLB ) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo . Ufafanuzi huo umetolewa jaa ( Ijumaa , Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari , Elimu na Mawasiliano wa HESLB , Dk Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ambako HESLB inashiriki katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara . “Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe ,” alisema Dk Mwaisobwa . Dk Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia kwa k...