Msanii diamond platnumz amezindua pafyum yake hii leo
Msanii wa muziki wa kizazi kipya , ambaye amekuwa akifanya vyema ndani na anga za Kimataifa Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato ( Pafyum ) yake iliyoitwa CHIBU , mapema leo jijini Dar. Wakati wa uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza manukato 'pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi . Amesema kuwa kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia , Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na...