Posts

Showing posts from April 19, 2017

Kati ya madaktari 500 walioombwa kwenda kenya 258 kuajiriwa Tanzania

Image
Rais John Magufuli amesema kati ya madaktari 500 walioonyesha nia ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya watachaguliwa 258 na kuajiriwa na serikali ya Tanzania mara moja kuanzia sasa. Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ilieleza kuwa hatua hiyo imefuatia baada ya kutetereka kwa makubalino ya serikali ya Tanzania na Kenya baada ya Mahakama nchini Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo. “Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na serikalini mara moja. Kufuatia uamuzi huu, majina ya madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya wizara www.ehealth.go.tz  pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo,” amesema Ummy

MILIKI BLOG YAKO SASA

Je unataka kuwa mmliki wa blog? KUTOKA TATA BLOG Hii ni fursa kwako kama mwanajamii mpenda maendeleo sasa unaweza kumiliki blog ambayo huenda ikawa na faida kubwa pindi tu   tutakapo kuunganisha na makampuni makubwa ya matangazo na kuanza   kutangaza na wewe . Huenda pia unahitaji blog kwaajili ya kuandaa taarifa zako na kuifanya kama diary yako kwani kwa sasa teknolojia imepanuka na imekua kubwa sana sio lazima utunze kumbukumbu kwenye vitabu   ambayo kesho huenda vikapotea au kuungua , miliki blog utunze kumbukumbu . Vilevile inawezekana wewe ni mjasiriamali na unhependa kutangaza biashara yako mbali zaidi ukiachana na makundi ya WhatsApp ambayo sio rahisi mtu   kuingia   kwenye engine search na kuziona bidhaa zako . kama hivyo basi karibu utengeneze blog ambayo itaonekana kwenye engene search na kukutangaza kirahisi . Vilevile labda unatak...

ISHU YA VYETI FEKI IMEICHUKUA SURA MPYA TENA

Image
Watumishi wa umma wafikia 10,000, Wamo mabalozi, wakuu wa wilaya, mikoa Na Fredy Azzah-DODOMA SEKESEKE la watumishi wa umma kushughi vyeti vya elimu limezidi kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000. Hatua hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao, 1,951 wana vyeti vya kughushi. Kuongezeka kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli, wiki iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali ambao wamebainika kuwa na vyeti feki. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki ni zaidi ya 9,000 na anaisubiri ripoti hiyo kuifanyia kazi. “Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo...