NYASA Mbamba bay barabara ni mbovu sana
Wakati watanzania maeneo mengine ya nchi wakipambana na swala la utawala bora, ufisadi na mengine kama hayo .wakiwa tayari wamesahau adha za barabara mbovu katika maeneo yao ,huko mkoani Ruvuma hali bado sio nzuri katika baadhi ya barabara zake kwani wananchi wanalazimika kujikwamua wawapo safarini ,barabara ni mbovu hasa barabara ya kuelekea Nyasa mbamba bay Ingawa hata katika maeneo ya katikati ya mji Wa SONGEA bado muonekano Wa barabara zake hauridhishi kutokana na kuwepo kwa mashimo katika kila barabara inayo katiza hapo mjini.