FAHAMU ELIMU YA TANZANIA BARA ILIVYOKUWA KABLA YA UHURU
Elimu ya Tanzania bara Kabla ya Uhuru Elimu ya Jadi: Historia ya Elimu Tanzania Bara imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni kabla na baada ya uhuru. Kabla ya kuja kwa wageni katika mwambao wa Tanganyika, kila kabila lilikuwa na mfumo wake wa elimu ya kijadi. Elimu ya Kijadi ilitokana na taratibu za kila siku za jamii za makabila mbalimbali. Elimu hiyo iliyojumuisha maarifa, stadi, maadili, utamaduni, mbinu na taratibu nzuri za kufanya kazi na kujilinda kutokana na mabaa ya njaa, magonjwa na maadui wa usalama wa jamii na wa mali zao ilirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mambo ya kujifunza yaligawanyika kirika na kutolewa na watu wazima nyumbani, kazini na katika nyanja nyingine za maisha. Mfumo huu ulianza kuwa na mabadiliko katika malengo na utoaji wake tangu wakoloni walipoingia nchini. Elimu Wakati wa Ukoloni: Wageni wa kwanza Tanzania Bara walikuwa Waarabu, wakifuatiwa na Wareno, Wajerumani na Waingereza. Kwa kuwa wageni hao...