Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi
UTANGULIZI Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu hizo ni utangulizi, kiini na hatimaye hitimisho. Katika utangulizi tumeweza kufafanua maana ya nadharia kwa kuwarejerea wataalamu mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa wameelezea vizuri maana ya nadharia. Wataalamu hao ni kama vile Masamba (2009), Sarantakos (1997), Martin E. Amin (2005). Lakini pia katika kiini tumeweza kujikita moja kwa moja na swali letu jinsi linavyotaka kuwa tutumie nadharia ya saikochanganuzi ili kuhakiki tamthiliya ya NGUZO MAMA. Hivyo katika sehemu hii ya kiini tumeweza kuonesha jinsi gani nadharia hii ya saikochanganuzi ilivyojidhihirisha kwenye kitabu cha NGUZO MAMA kutokana na wahusika mbalimbali kama vile Bi moja, Bi pili, Bi tatu, Bi nne, Bi tano, Bi sita, Bi saba, Bi nane na wahusika wengineo kama chizi. Hivyo basi katika kazi yetu tumeweza pia kuhitimisha kazi kwa kutoa mawazo kuwa ni jinsi gani wanawake wa patata wameweza kupambana vikali dhidi ya kuinua NGUZO MAMA kwa kuanzisha miradi mbalim...