Posts

Showing posts from April 3, 2017

Magazeti ya leo jumanne

Image
Magazeti Ya Leo Jumanne ya April 4

Bunge kuanza leo ,tizama ratiba ya leo

Image
Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017

Bunge lagomea wapinzani kugombea ubunge

Image
Bunge Lakataa majina ya wagombea wa CHADEMA na CUF kwenda kugombea nafasi ya Ubunge wa Afrika Mashariki ( EALA Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekataa majina ya wagombea wa CHADEMA na CUF kwenda kugombea nafasi ya Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA) baada ya kukutwa na mapungufu katika fomu zao. Hatua hiyo imekuja baada ya wagombea hao kuonekana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwenye nyaraka zao a uteuzi yakiwa yamekiuka masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki ya Mwaka 2011 iliyotungwa na Bunge la Afrika Mashariki. Aidha taarifa hiyo imesema CHADEMA uteuzi wao haukuzingatia jinsia, lakini pia hawajaambatanisha fomu za maombi ya wagombea, orodha ya waombaji pamoja na fomu ya matokeo ya kura. Huku CUF wakiwa wametuma fomu za uteuzi wa wagombea zikiwa zimewasilishwa na mamlaka mbili tofauti...

Dr.KIGWANGALA asema haya

Hata siku moja usipende kuiga, fanya lako-shika safari yako kwa spidi yako; usiige mbio za wengine hujui wanatoka wapi na wanaenda wapi!

HARMORAPA

'Nilijisikia vibaya sana, kwa nini watu wanajaribu kunirushia chupa, sijui kwa lengo gani? ikiwa mimi natafuta' Harmorapa ayanena hayo Mara baada ya show yake.

China yapiga marufuku ndevu

Image
CHINA: Serikali yapiga marufuku wanaume Waislamu kufuga ndevu ndefu na wanawake kuvaa hijab huko eneo la Xinjiang lenye Waislamu milioni 10.

ALIYE TUMBULIWA SASA NYOTA IMENG'AA

Image
Aliyetumbuliwa na Rais Magufuli Dk Mwele Malecela Ateuliwa Kuwa Mkurugenzi Shirika la Afya Duniani (WHO) Salamu za pongezi zimeendelea kumiminika kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika. Pia, Dk Mwele  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville.  Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020, una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa.  Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na usubi.  Miongoni mwa waliomtumia pongezi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Sikika, Irenei Kiria ambaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: “Hongera Mwele ...

ZITO KABWE AGONGA MWAMBA

Image
Zitto Kabwe Agonga Mwamba Ubunge ELA....... Spika Ndugai Agomea Maombi Yake Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),  amegonga mwamba baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kutoa msimamo wake kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Hatua hiyo inatokana na Zitto kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Machi 28, mwaka huu akitaka kamati hiyo kutoa ufafanuzi wa mgombe wa kundi C ili kila chama kiweze kushiriki uchaguzi, badala ya kupewa kwa vyama vilivyokuwa na idadi kubwa ya wabunge. Kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, Zitto, alisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na si uchaguzi. Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotaka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo, lakini pia inavinyima vyama v...