Posts

KILELE CHA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WANAWAKE WA AJUCO

Image
Uzinduzi kampeni ya kumkomboa mtoto Wa kike  kwa kumpatia elimu ya kutosha ili kumfanya  aondokane na manyanyaso yanayomfanya mtoto Wa kike  kushindwa kupata elimu . "Nafurahi sana kwa kuwa nasi tumepata kuonekana ni watu katika jumuiya ya wanaAJUCO kwani haikuwahi kutokea  tukio kubwa la  namna ya pekeee lenye kuonyesha kutaka kuwakomboa wanawake  ,hasa  watoto wakike ambao bado wanaendelea  kupata elimu ya msingi ,sekondari na hata chuo kikuu ,nashukuru sana  kwa kitendo cha uungwana uliofanywa na wanawake  wa  jumuiya ya AJUCO kwani wanania njema ya kumkomboa mtoto Wa kike  aweze kupata elimu hadi ya ngazi za juu  .mmoja wa wanajumuiya ya AJUCO alisema hayo alipokuwa Akizungumza na tata blog pamoja na tata you tube channel

Waziri mwakyembe apiga marufuku kusomwa kwa magazeti katika redio na televisheni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.   Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia.   Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC

Marekani waanza upya kuichokonoa korea

Image
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea. Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini. Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini. Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang. Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera. Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi

Mbunge wa kawe Halima mdee asimamishwa rasmi kutohudhuria vikao ...zaidi soma hapa

Image
Mbunge wa jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee amepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vya bajeti katika bunge linaloendele hivi sasa Dodoma kufuatia Mbunge huyo kubainika kuwa alitukana bungeni, lakini Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani amesamehewa.  Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Mhe. Freeman Mbowe kwa kudharau mamlaka ya spika na kumsamehe kosa lake hilo kwa kile lichosema kuwa lilikuwa ni kosa la kwanza kwa kiongozi huyo kufanya.  Akisoma uamuzi huo, mjumbe wa kamati, Almasi Maige amesema Bunge lijadili na kutoa uamuzi kwa kiongozi huyo kusamehewa kwa sababu ni kosa la kwanza na aliitikia wito bila usumbufu na aliomba radhi, hivyo bunge limeazimia kumsamehe.  Mambo yamekuwa magumu kwa kwa upande wa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ambapo bunge limeazimia mbunge huyo kutohudhuria vikao vya bunge la bajeti vyote vinavoendelea sasa kwa kosa lake la kumtukana Spika na Mbunge akiwa bungeni.  Halima...

ACT WAZALENDO NA VYETI FEKI

Image
CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeitaka Serikali kufanya uhakiki wa vyeti kwa viongozi wote wa siasa na isipofanya hivyo kitafikisha suala hilo mahakamani. Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema endapo Serikali haitawahakiki viongozi hao na mamlaka zinazohusika kutowachukulia hatua kwa kughushi vyeti, kitafungua mashtaka mahakamani. “Malalamiko ya wananchi kuwa kuna viongozi  wamatumia vyeti feki na wengine wakituhumiwa kuwa na shahada batili ni ya muda mrefu. “Ikumbukwe kiongozi ni kama dereva kwa hiyo kuwaacha kwa kisingizio cha kujua kusoma na kuandika ni sawa na kuwa na dereva ‘kihiyo’ anayeendesha gari lililo na abiria waelewa,” alisema Shaibu. Alisema kitendo cha kutowahakiki viongozi hao kinapotosha mantiki nzima ya mchakato wa uhakiki na kuweka upendeleo wa dhahiri baina ya watumishi wa umma. “Msingi wa mchakato huu ni kuhakikisha t...

LOWASA AYASEMA HAYA KUHUSU JINA LA MWANAE KUWA KATIKA LISTI YA WENYE VYETI FEKI

Image
Toka jana habari inayo Gonga vichwa vya watu ni kuhusu vyeti feki kubwa zaidi ni Pale Jina la mtoto wa Lowassa kuwemo kwenye List ya wenye vyeti feki kiendo ambacho kime Mfedhehesha sana Lowassa na kusema kuwa Hata lifumbia macho hili swala la Mwanaye kuwekwa kwenye List ya vyeti feki Lowassa Nitalitolea Ufafanuzi Jina la Godfrey Ngoyai Lowassa lililopo kwenye list ya watu wenye vyeti feki Muda sio Mrefu

VYUO VYA UALIMU VYA KARABATIWA

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila     Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA SERIKALI imekarabati vyuo 10 vya ualimu kati ya 35 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia walimu. Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila, alipofungua mafunzo ya mradi wa kuimarisha elimu ya ualimu. “Hawa wanabeba jukumu kubwa la kuwasaidia watoto wetu, hivyo ni lazima Serikali iwaangalie na ndiyo maana tukakarabati vyuo 10 na hivi vingine vitaingia katika bajeti inayofuata,’’ alisema. Pia alisema wameamua kutoa mafunzo hayo ili wakuu wa vyuo wajue namna bora ya kufanya ununuzi katika vitu mbalimbali.  “Katika ununuzi kuna utaratibu wa kufuata, kila kinachonunuliwa lazima thamani ya fedha ionekane, sio unakurupuka tu kujinunulia, lazima uangalie na bei ya soko ikoje.  “Mradi huu utakuwa ni wa miaka mit...