Posts

RAIS ZUMA ATAKA ZIWA VICTORIA LIBADILISHWE JINA

Image
.  Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo. Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo. Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria. Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema  Ziwa hilo kuendelea kuitwa  Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao. “Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango  dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma

Mwanafunzi akishitaki chuo kikuu cha UDSM

Image
Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Alphonce Lusako, amewasilisha maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, aruhusiwe kukishtaki chuo hicho kwa kumkatisha masomo. Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya sheria alifukuzwa baada ya kufutiwa usajili Januari 26, pamoja na mambo mengine akidaiwa kusajiliwa kwa makosa kwasababu aliwahi kufukuzwa chuoni hapo. Lusako anayewakilishwa na Wakili Jebra Kambole anaiomba Mahakama impe kibali cha kuishtaki UDSM na itoe amri ya kuzuia uamuzi wa kumfutia usajili. Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Mei 23 na Jaji Pellagia Khaday. Lusako alijiunga na UDSM kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akiwa amedahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu. Hii ni mara ya pili kwa Lusako kufukuzwa chuoni hapo, mara ya kwanza ni Desemba 13, 2011, pamoja na wenzake kadhaa, akiwa mwaka wa tatu walifukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu nchini wakidaiwa kuratibu mgomo wa wanafunzi UDSM. Hata hivyo, anadaiwa alikuwa akip...

BENKI KUU YA TANZANIA IMEAMUA KUIFUTIA LESENI BENK MOJA HAPA NCHINI zaidi soma hapa

Image
Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016. Aidha Benki Kuu ya Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza. Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake. “Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza. Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.” Benk...

KILELE CHA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WANAWAKE WA AJUCO

Image
Uzinduzi kampeni ya kumkomboa mtoto Wa kike  kwa kumpatia elimu ya kutosha ili kumfanya  aondokane na manyanyaso yanayomfanya mtoto Wa kike  kushindwa kupata elimu . "Nafurahi sana kwa kuwa nasi tumepata kuonekana ni watu katika jumuiya ya wanaAJUCO kwani haikuwahi kutokea  tukio kubwa la  namna ya pekeee lenye kuonyesha kutaka kuwakomboa wanawake  ,hasa  watoto wakike ambao bado wanaendelea  kupata elimu ya msingi ,sekondari na hata chuo kikuu ,nashukuru sana  kwa kitendo cha uungwana uliofanywa na wanawake  wa  jumuiya ya AJUCO kwani wanania njema ya kumkomboa mtoto Wa kike  aweze kupata elimu hadi ya ngazi za juu  .mmoja wa wanajumuiya ya AJUCO alisema hayo alipokuwa Akizungumza na tata blog pamoja na tata you tube channel

Waziri mwakyembe apiga marufuku kusomwa kwa magazeti katika redio na televisheni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.   Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia.   Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC

Marekani waanza upya kuichokonoa korea

Image
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea. Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini. Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini. Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang. Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera. Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi

Mbunge wa kawe Halima mdee asimamishwa rasmi kutohudhuria vikao ...zaidi soma hapa

Image
Mbunge wa jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee amepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vya bajeti katika bunge linaloendele hivi sasa Dodoma kufuatia Mbunge huyo kubainika kuwa alitukana bungeni, lakini Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani amesamehewa.  Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Mhe. Freeman Mbowe kwa kudharau mamlaka ya spika na kumsamehe kosa lake hilo kwa kile lichosema kuwa lilikuwa ni kosa la kwanza kwa kiongozi huyo kufanya.  Akisoma uamuzi huo, mjumbe wa kamati, Almasi Maige amesema Bunge lijadili na kutoa uamuzi kwa kiongozi huyo kusamehewa kwa sababu ni kosa la kwanza na aliitikia wito bila usumbufu na aliomba radhi, hivyo bunge limeazimia kumsamehe.  Mambo yamekuwa magumu kwa kwa upande wa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ambapo bunge limeazimia mbunge huyo kutohudhuria vikao vya bunge la bajeti vyote vinavoendelea sasa kwa kosa lake la kumtukana Spika na Mbunge akiwa bungeni.  Halima...