Posts

WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA SHULE MBALIMBALI ZA ADVANCE TAZAMA HAPA

http://tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/

GWAJIMA ALIAMSHA TENA DUDE

Tazama askofu gwajima alivyoliamsha dude linalimhusu Bashite nenda moja kwamoja kwenye VIDEO UTAZAME

Tembelea TATA BLOG utazame videos mbalimbali kuanzia sasa

Tazama video mbalimbali katika blog yetu kadri uwezavyo

UNAFAHAMU WIZARA ILIYOBADILISHA MAWAZIRI WENGI KULIKO WIZARA ZINGINE ?

                                                                        Na tatablog    Wizara ya Nishati na Madini ni miongoni mwa wizara ya zamani sana hapa nchini, ilianzishwa mara tu baada ya kupata uhuru mwaka 1961. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nchi hii ilikuwa ikifanya shughuli za uchimbaji madini pamoja na za nishati – kama vile usambazaji wa umeme na uagizaji wa mafuta ya magari na mitambo. Hata hivyo katika miaka ya karibuni wizara hiyo imetokea kuwa miongoni mwa wizara zenye misukosuko mikubwa kiasi kwamba mawaziri wanaoteuliwa kuiongoza huwa hawakai muda mrefu. Waziri atakayeteuliwa kumrithi Prof Sospeter Muhongo aliyeondolewa kwenye wadhifa huo wiki iliyopita ata kuwa ni wa nane kushika wizara hiyo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Wizara nyingine ambazo pia zimekuwa zikib...

RAIS ZUMA ATAKA ZIWA VICTORIA LIBADILISHWE JINA

Image
.  Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo. Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo. Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria. Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema  Ziwa hilo kuendelea kuitwa  Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao. “Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango  dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma

Mwanafunzi akishitaki chuo kikuu cha UDSM

Image
Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Alphonce Lusako, amewasilisha maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, aruhusiwe kukishtaki chuo hicho kwa kumkatisha masomo. Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya sheria alifukuzwa baada ya kufutiwa usajili Januari 26, pamoja na mambo mengine akidaiwa kusajiliwa kwa makosa kwasababu aliwahi kufukuzwa chuoni hapo. Lusako anayewakilishwa na Wakili Jebra Kambole anaiomba Mahakama impe kibali cha kuishtaki UDSM na itoe amri ya kuzuia uamuzi wa kumfutia usajili. Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Mei 23 na Jaji Pellagia Khaday. Lusako alijiunga na UDSM kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akiwa amedahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu. Hii ni mara ya pili kwa Lusako kufukuzwa chuoni hapo, mara ya kwanza ni Desemba 13, 2011, pamoja na wenzake kadhaa, akiwa mwaka wa tatu walifukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu nchini wakidaiwa kuratibu mgomo wa wanafunzi UDSM. Hata hivyo, anadaiwa alikuwa akip...

BENKI KUU YA TANZANIA IMEAMUA KUIFUTIA LESENI BENK MOJA HAPA NCHINI zaidi soma hapa

Image
Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016. Aidha Benki Kuu ya Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza. Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake. “Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza. Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.” Benk...