UNAFAHAMU WIZARA ILIYOBADILISHA MAWAZIRI WENGI KULIKO WIZARA ZINGINE ?

                                                                       Na tatablog 
 Wizara ya Nishati na Madini ni miongoni mwa wizara ya zamani sana hapa nchini, ilianzishwa mara tu baada ya kupata uhuru mwaka 1961. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nchi hii ilikuwa ikifanya shughuli za uchimbaji madini pamoja na za nishati – kama vile usambazaji wa umeme na uagizaji wa mafuta ya magari na mitambo. Hata hivyo katika miaka ya karibuni wizara hiyo imetokea kuwa miongoni mwa wizara zenye misukosuko mikubwa kiasi kwamba mawaziri wanaoteuliwa kuiongoza huwa hawakai muda mrefu. Waziri atakayeteuliwa kumrithi Prof Sospeter Muhongo aliyeondolewa kwenye wadhifa huo wiki iliyopita ata kuwa ni wa nane kushika wizara hiyo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Wizara nyingine ambazo pia zimekuwa zikibadilishwa mawaziri mara kwa mara ni ile ya Mambo ya Ndani na Maliasili na Utalii. Hivyo tangu uhuru kumekuwepo jumla ya mawaziri 25 ingawa baadhi yao (watatu) walirudia kuiongoza wizara hiyo kwa mara ya pili na mmoja mara tatu. Watanzania mashuhuri waliowahi kuongoza wizara hiyo ni pamoja na John Malecela aliyeongoza tangu 1980 hadi 1981, Paul Bomani (1983-84) na Alnoor Kassum katika vipindi vitatu vifupi vifupi — mwaka 1980, 1984 na baadaye 1985. Mtu mashuhuri zaidi kuiongoza wizara hiyo ni aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuanzia 1990 had 1995. Mawaziri waliorudua kuiongoza wizara hiyo ni Alnoor Kassum I(mara tatu), Jackson Makwetta (mara mbili), Edgar Maokola Majogo (mara 2) na Pro Sospeter Muhongo (mara mbili). Hata hivyo iwapo Professor Muhongo angewahi kujiuzulu kutoka Wizara hiyo wiki iliyopita kabla ya rais John Mafufuli kutengua uteuzi wake, basi angekuwa ni waziri pekee hapa nchini kujiuzulu mara mbili kutoka wizara moja katika vipindi tofauti. Mtanzania wa kwanza kuongoza wizara hiyo alikuwa Amir H. Jamal mwaka 1961 wakati ule ikiitwa Wizara ya Biashara, Madini na Nguvu za Umeme. Jina hili liliendelea hadi wizara ilipobadilishwa na kuitwa Wizara ya Maji na Nguvu za umeme mwaka 1970 ambapo mwaka 1975 ikawa Wizara ya Naji, Nishati na Madini. Sasa hivi inaitwa Wizara ya Nishati na Madini na mtu wa kwanza kuiongoza chini ya jina hilo ni Dk Idrisa Msabaha chini ya Rais Jakaya Kikwete, akifuatiwa na Nazir Karamagi. Ilikuwa ni katika kipindi hiki cha Karamagi ndipo kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond ilipoitikisa nchi. Harakati za kutafuta umeme wa kuaminika iliilazimu serikali kuingia mikataba ya kufua umeme na makampuni ya kutoka nje. Hata hivyo baadaye ikaja kugundulika kuwa Richmond ilikuwa kampuni hewa na kutokana na kelele kutoka Bungeni Waziri Karamagi, na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa. Aliyekuwa Naibu Waziri William Ngeleja ndiye alkimrithi Karamagi, ambaye mwaka 2912 aliondolewa, pamoja na mawaziri wengine kadha, kutokana na utendaji kazi wao usioridhisha. Lakini pengine hakuna waziri aliyepata misukosuko mikubwa katika wizara hiyo, kama Pro Muhongo ambaye katika kipindi chake cha awali chini ya Kikwete ndiyo uwepo wa gesi asilia katika maeneo ya kusini mwa Tanzania katika ukanda wa bahari kulitangazwa kupatikana kwa wingi. Profesa Muhongo alikuwa ni mmoja wa mawaziri maarufu aliyesomea elimu ya miamba, hivyo elimu yake iliendana na wadhifa aliopewa, ingawa alikuwa mgeni katika siasa. Kwa mara ya kwanza aliteuliwa kuwa mbunge na baadaye waziri wa wizara hiyo na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2012. Alifikia kilele cha umaarufu wake mwaka miaka mitatu iliyopita 2014, kwa kujizolea sifa katika kuzungumza kwa kutumia takwimu na pasipo woga au kutafuna maneno. Lakini pamoja na sifa hizi Prof Muhongo baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu akaja kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kashfa ya Escrow, mapema mwaka 2015. Katika hali hii uteuzi wake kwa mara ya pili kushika wadhifa huo na rais magufuli miezi 11 tu baadaye haukupokelewa vyema na baadhi ya wananchi. Wengi waliona kwamba Muhongo hakufanya ufisadi wowote katika kashfa hiyo ya uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania isipokuwa aliwajibika kisiasa kwani madudu ya kashfa hiyo yalitendeka chini ya usimamizi wake. Wengine walisema Rais Magufuli alikosea sana kumrejesha katika wizara ambayo alionekana amevurunda huko nyuma. Hawa wanataja tukio moja ambalo lingemfanya Rais Magufuli kumuondoa Prof Muhongo mapema zaidi kuliko alivyofanya – tukio lile la mita za kupimia mafuta yanyoagizwa kutoka nje. Mapema 2016 Prof Muhongo alidaiwa kupeleka ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa Mkuu wa kitengo cha Vipimo (Weights and Measures) kilichopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kumtonya kwamba waziri Mkuu atatembelea kituo cha upakuaji mafuta kule Kurasini hivyo ahakikishe zile mita zinafunguliwa. Pamoja na tukio hili Magufuli alimwacha tu. Mawaziri walioongoiza Wizara ya Nishati na Madini tangu 1961:   A. H. Jamal (1961-64) A. K. E. Hanga (1964) J. S. Kasambala (1964 -1965) A. Z. Nsilo Swai (1966-70) I. Elinawinga (1970-75 W. K. Chagula (1975-1980) Alnoor Kassum (1980) John Samwel Malecela(1980-1982) Jackson Makweta (1983) Paul Bomani (1983-1984) Alnoor Kassum (1984) Pius Y. Ng’wandu (1984-85) Alnoor Kassum (1985) Edgar Maokola Majogo (1985-1988) Jakaya Kikwete (1990-1995) Jackson M. Makweta (1995) Ernest Nyanda (1990-1991) Joseph Mbwiliza (1991-1995) William Shija (1995–1996) Abdallah Omari Kigoda (1996–2001) Edgar Diones Maokola Majogo (2002) Daniel Yona (2002-2006) Ibrahim Msabaha (2006-2007) Nazir Mustafa Karamagi (2007-2008) William Mganga Ngeleja (2008–2012) Prof. Sospeter Muhongo (2012–2014 George Simbachawene 2014–2016 Prof Sospeter Muhuongo 2017–2017.     The post NISHATI NA MADINI: WIZARA ILIYOBADILISHA MAWAZIRI WENGI KULIKO NYINGINE 

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi