JUMA NKAMIA AZUNGUMZIA SWALA LA WAZIRI WA HABARI KUHUDHURIA KWENYE MKUTANO WA MWANAMUZIKI ZAIDI SOMA HAPA

Mbunge Wa chemba Mh Juma Nkamia alipopata nafasi ya kusimama bungeni amezungumzia kuhusu swala La Waziri Wa habari utamaduni na Michezo kuhudhuria mkutano Wa mwanamuziki Roma aliyetekwa hivi karibuni ,Nkamia

Amesema: Jana nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza, Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma atakataa?

"Mtu alitekwa, serikali ndo inamwandalia press conference na kuisimamia? Ivi kesho mkiambiwa ndo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma, lakini lazima tuseme.

"Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.

"Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri.....No, lazima tuseme ukweli

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi