HISTORIA FUPI IKIMUHUSISHA MAREHEMU CHANDE KIONGOZI WAO
Mtego wa Freemasons ulikua hivi Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.
Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.
Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.
Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.
Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.
“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.
Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.
Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.
Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.
Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.
“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.
Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.
Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Kanuni za Freemason zinafundisha nini?
Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.
“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.
Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.
Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.
“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:
“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na...Chande amefariki wakati akipata matibabu katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri miaka 88 baada ya kuugua kwa muda mrefuna mwili wake umechomwa moto jijini DAR ES SALAAM
Comments