MAREKANI VS KOREA KUSINI


Ndege za jeshi la Marekani aina ya B-1B zikipaa juu ya Pyeongtaek, Korea Kusini 13 Septemba, 2016. 

Ndege mbili za kivita za Marekani zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia, B-1 Lancer, zimepaa juu ya anga ya Korea Kusini, siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la tano la silaha za nyuklia.

Ndege hizo zilipaa si mbali sana kutoka ardhini juu ya kituo cha kijeshi kinachopatikana kilomita 77 kutoka mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Marekani imeitahadharisha Korea Kaskazini kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taifa hilo baada ya kufanyika kwa majaribio hayo ya bomu Ijumaa.

Jaribio hilo la Pyongyang ndilo kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na taifa hilo.

'Ndege aina ya B-1 zina uwezo wa kubeba makombora yenye mabomu ya nyuklia au mabomu ya nyuklia yenyewe yenye uwezo wa kuharibu hata mahandaki.
Kamanda wa jeshi la Marekani eneo la Korea Jenerali Vincent Brooks (pili kutoka kulia) amesema hatua ya Pyongyang imezidisha hali ya wasiwasi eneo hilo. 

Operesheni hiyo ya kupaa kwa ndege ilikuwa imepangiwa kufanyika Jumatatu lakini ikacheleweshwa kutokana na hali mbaya ya hewa Guam, eneo ambalo ndege hizo hukaa.

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi