Fahamu sasa kuwa mbu amewazidi ujanja wataalamu
Kwa vipi? Inaelezwa kwamba mbu nchini hapa sasa anaishi kwa muda mrefu zaidi na kutaga mayai yao katika sehemu za wazi chini ya ardhi.
Ugunduzi huo unaleta tafsiri mpya kwamba sasa hatari ya maradhi yatokanayo na mbu kuwa ni makubwa zaidi, hasa kwa magonjwa kama matende, malaria na zika ambayo ni tishio kubwa katika baadhi ya nchi.
Hiyo sasa inazaa changamoto mpya ya haja ya kufanyika utafiti zaidi kukabli kasoro hiyo ambayo ni mzizi wa janga la hatari kwa afya watu.
Mtaalamu Dk. Moritz Kraemar, anasema takwimu za hivi sasa duniani kunabashiriwa kuwepo watu bilioni 2.17 wanaoishi katika maeneo hatari ya kuambukizwa na maradhi yatokanayo na mbu, huku katika baadhi ya nchi kama vile Jamaica, wameanza kubuni njia mpya ya kukabili kasoro hiyo tishio.
Pia, utafiti umegundua hatari ya kuwepo mbu wanaozaliana kwa wingi zaidi, iko katika maeneo ya joto, kuliko kwenye baridi zaidi. Kwa maana hiyo, makazi ya watu kwenye baridi sasa ndio kuko jirani na majanga ya kiafya yatokanayo na mbu.
Mbali na hilo, pia uhai wa mbu ambao ulizoeleka kwamba wanaishi wastani wa siku 30 tu, sasa wameibuka kuwa na uhai zaidi wakiwepo wanaodumu kwa siku 100 au sawa na miezi na wiki moja na nusu, ambayo ni zaidi ya mara tatu ya uhai uliozoeleka.
Kutokana na mustakabali huo uliofafanuliwa, Mtafiti Sebastian Gourbiere, anashauri kwamba kuna haja ya nchi mbalimbali kufanya mapitio mapya ya namna ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mbu.
Ni utafiti unaotokana na mwitikio wa wito kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), uliozitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua haraka ya kuyafuatilia kwa karibu maradhi mbalimbali ambayo si ya kuambukiza baina ya mtu mmoja na mwingine, ikiwemo Zika iliyogonga hodi katika nchi zisizopungua 149 duniani.
Mapungufu hayo yanayoelezwa kutoka kwa mbu yakifanyiwa masihara, kuna hatari kuwa maradhi kama Zika yatasambaa kwa kasi na kubwa na kuwa janga la kimataifa.
Timu ya wataalamu wanaoongozwa na Dk. Moritz Kraemer, inafafanua kwamba kwa hali ilivyo sasa, maradhi kama Zika yakifanyiwa masihara, yana hatari ya kufika pabaya hata kutokomeza theluthi moja ya wakazi wa dunia.
Inaelezwa kwamba mbu hao wana uwezo wa kumaliza mazingira bora kwao kuishi, kutoka sehemu moja hadi nyingine, hata yakiwepo mabadiliko ya hali ya hewa na kwa maana hiyo, inakuwa rahisi kwao kuasambaza maradhi kwa njia ya kuambukiza kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Comments