Aliye muweka mpenzi wake kwenye jaba la maji sasa mikononi mwa..,zaidi soma hapa

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.

Sirro ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi