Mwanafunzi na msanii Dax aweka wazi safari ya maisha yake kwa wana AJUCO yakwamba hii Leo anatimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa
Happy born day brother dax
UTANGULIZI Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu hizo ni utangulizi, kiini na hatimaye hitimisho. Katika utangulizi tumeweza kufafanua maana ya nadharia kwa kuwarejerea wataalamu mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa wameelezea vizuri maana ya nadharia. Wataalamu hao ni kama vile Masamba (2009), Sarantakos (1997), Martin E. Amin (2005). Lakini pia katika kiini tumeweza kujikita moja kwa moja na swali letu jinsi linavyotaka kuwa tutumie nadharia ya saikochanganuzi ili kuhakiki tamthiliya ya NGUZO MAMA. Hivyo katika sehemu hii ya kiini tumeweza kuonesha jinsi gani nadharia hii ya saikochanganuzi ilivyojidhihirisha kwenye kitabu cha NGUZO MAMA kutokana na wahusika mbalimbali kama vile Bi moja, Bi pili, Bi tatu, Bi nne, Bi tano, Bi sita, Bi saba, Bi nane na wahusika wengineo kama chizi. Hivyo basi katika kazi yetu tumeweza pia kuhitimisha kazi kwa kutoa mawazo kuwa ni jinsi gani wanawake wa patata wameweza kupambana vikali dhidi ya kuinua NGUZO MAMA kwa kuanzisha miradi mbalim...
Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia. MPANGO KAZI Katika kazi hii, tumelenga kufafanua dhana ya tamthiliya, dhana ya tanzia pamoja na istilahi za msingi katika tamthiliya ya tanzia. Pia kazi yetu imegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani Utangulizi, kiini cha swali, na hitimisho. Katika sehemu ya utangulizi tumejadili dhana ya tamthiliya na tanzia kwa kurejea wataalamu mbalimbali kama vile, TUKI, (2004), Mlama, (1983:203) katika dhana ya tamthiliya. Katika dhana ya tanzia tumeweza kuwatumia wataalamu kama vile Semzaba, (1997) Katika sehemu ya pili ambayo ni kiini cha swali hapa tumeweza kujadili istilahi mbalimbali za msingi katika tamthiliya ya tanzia. Vilevile katika sehemu ya mwisho ambayo ni hitimisho tumeweka mawazo ya jumla ya kazi yetu. UTANGULIZI. Maana ya tamthiliya. Kwa mujibu wa TUKI, (2004). Tamtiliya ni utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo. Tamthiliya ni sanaa ya maonyesho, sa...
DHANA YA MOFU NA AINA ZAKE TUKI(1990), katika Dafina ya Lugha wanasema kuwa, “Mofu ni kipashio cha isimu maumbo kiwakilishacho mofimu”. Massamba (2004), katika Dafina ya Lugha anasema , Mofu ni kipashio cha kimaumbo ambacho huwakilisha mofimu. Kwa mujibu wa Nida (1949), wanasema, Mofu ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu na ambalo huthihirika kifonolojia na kiothografia. Mofu ni kipashio kidogo kabisa chenye maana katika lugha.Mofu hawezi kugawanywa katika sehemu ndogo zaidi bila kuharibu maana yake. Mofu huwakilisha maana za kileksika na zile za kisarufi. (Platt,1985). Kwa ujumla, Mofu ni kipashio cha kimofolojia ambacho husitiri maana za mofimu katika lugha na huweza kudhihilika kifonolojia zinapotamkwa na kiothografia zinapoandikwa katika lugha. Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili; Kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu na Kigezo cha mofolojia ya mofu. Tunapotumia kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu, tunapata aina tatu za mofu, yaani; mofu hu...
Comments