FAHAMU HAYA KUHUSU UJAUZITO WA LINNAH

March 31 2017 kupitia kipindi cha The weekend chat show Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amekiri alishawahi kutoa mimba takribani mbili kabla ya hii aliyonayo sasa hivi na anategemea kujifungua hivi karibu.

Linah amesema anajutia hilo na sababu iliyompelekea kutoa mimba hizo ni kwa sababu alikuwa anamuhofia baba yake kwakuwa hakuwa ameolewa na kudai baba yake alisha watahadharisha juu ya kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa wajitenge wenyewe kwenye familia yao.

Mtangazaji Soudy Brown alimuuliza Linah kama alishawai kutoa Mimba na majibu yake yalikuwa haya..>>>“Yah nisiwe muongo nilishawahi kutoa mimba kipindi cha nyuma, nilikuwa naogopa kwasababu Baba yangu alikataa mtu kubeba mimba nje ya ndoa”

“Mimba nimezitoa, siyo mara nyingi ila naweza kusema kama mara mbilii”:-Linah

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi