Kati ya madaktari 500 walioombwa kwenda kenya 258 kuajiriwa Tanzania

Rais John Magufuli amesema kati ya madaktari 500 walioonyesha nia ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya watachaguliwa 258 na kuajiriwa na serikali ya Tanzania mara moja kuanzia sasa.

Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ilieleza kuwa hatua hiyo imefuatia baada ya kutetereka kwa makubalino ya serikali ya Tanzania na Kenya baada ya Mahakama nchini Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo.

“Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na serikalini mara moja. Kufuatia uamuzi huu, majina ya madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya wizarawww.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo,” amesema Ummy

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi