Tamasha la Bodaboda kutikisa Dar, Bodaboda 5000 kuchuana Mei 13
Kufuatia usafiri wa bodaboda kuongoza kwa usababishaji wa ajali barabarani zinazopelekea watu wengi kupoteza maisha na au kuwa walemavu wa kudumu, pamoja na kuhusishwa na matukio ya uhalifu hapa nchini.
Kampuni ya JP Decaux na Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya maendeleo katika jamii IRI, wameandaa tamasha maalumu kwa wadau wa sekta ya bodaboda linaloitwa ‘DAR BODABODA SUPERSTAR UNITY FESTIVAL’ ambalo limelenga kutoa semina za umuhimu wa uendeshaji ulio salama kwa kuzingatia sheria za barabarani na umuhimu wa matumizi ya bima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Tamasha hilo, Anna Saggi amesema kuwa litafanyika Mei 13, 2017 katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe Jijini Dar es Salaam kuanzia.
“Lengo la tamasha hili ni kuweka uamsho na msisitizo wa wa utolewaji wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa dhumuni la kuzingatia sheria za usalama barabarani. Pia limelenga kudumisha umoja na ushirikiano katika jamii. Litafanyika kila mwaka ambapo mwaka huu watu Zaidi ya 5000 wanatarajia kushiriki,” amesema.
Comments