Upinzani kenya waruhusiwa kujihesabia kura ...zaidi soma kwenye tata blog

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imekubali hitaji la vyama vya kisiasa kujihesabia kura katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika Agosti 8, mwaka huu.

Hata hivyo, licha ya ruhusa hiyo tume hiyo imesema kuwa ni yenyewe pekee yenye ruhusa na mamlaka ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Awali Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa NASA, utaratibu kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Viongozi wa upinzani wanasema kuwa uwepo wa kituo hicho utasaidia kuzuia udanganyifu katika uchaguzi huo.

Rais Uhuru Kenyatta anawania muhula wa pili wa uongozi wake na anatarajia kuukabili muungano wa vyama vikuu vya upinzani.

Uamuzi wa tume ya uchaguzi Kenya umekuwa tofauti na ilivyokuwa Tanzania ambapo Muungano wa Vyama vya Upinzani ‘UKAWA’ ulibuni kituo chake cha kuhesabia kura lakini hakikuruhusiwa kufanya kazi yake hadi mwisho huku baadhi ya wahusika wakitiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani

Comments

Popular posts from this blog

Kwa kutumia mifano jadili istilahi muhimu katika tamthiliya ya tanzia.

ZIFAHAMU METHALI ZA KISWAHILI ZIPATAZO 600 NA ZAIDI

Uhakiki wa tamthiliya ya nguzo mama kwa kutumia nadharia ya saikochanganuzi